WEDNESDAY NIGHT LIVE: Kilichojificha nyuma ya mafanikio ya soka la vijana Tanzania


Wiki hii kipindi cha Wednesday Night Live kimelimulika soka la vijana Tanzania kwa kuangalia mambo yanayofanyika nyuma ya pazia na kuifanya Tanzania kung’ara kwenye soka la vijana Afrika Mashariki na Kati pamoja na Afrika kwa ujumla kupitia kikosi cha Serengeti Boys. Pia kipindi hiki kimeyatazama kiufundi maandalizi ya michuano ya AFCON kwa vijana ambayo itafanyika hapa nchini Tanzania, pamoja na mashindano ya kufuzu fainali hizo yaliyofanyika hapa nchini na Serengeti Boys kuambulia nafasi ya tatu. Patrick Nyembera anazungumza na makocha wawili wa timu za vijana ambao ni Oscar Milambo ambaye ndiye kocha wa Serengeti Boys pamoja na Peter Manyika ambaye ni kocha wa makipa wa timu za vijana. Wednesday Night Live ni kila Jumatano saa 3:30 usiku, Azam Sports 2.


No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.