Okwi Mfungaji Bora Ila Kashindwa Kuvunja Rekodi Hii.


Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameibuka kuwa mfungai bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu baada ya kufunga mabao 20.

Licha ya kuibuka kinara wa upachikaji wa mabo Okwi ameshindwa kuivunja rekodi ya Murundi, Amis Tambwe ambaye alimaliza msimu wa 2015/2016 kwa kupachika kimiani jumla ya magoli 21 akiwa na klabu yake ya sasa ya Yanga sc.

Okwi anafuatiwa na Marcelo Kaheza na John Bocco wote wakiwa na mabao 14. Kaheza anatarajiwa kuichezea Simba kuanzia msimu ujao.

Anayeshika nafasi ya nne ni mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa mwenye mabao 12 akifuatiwa na Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao 10.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.