TAARIFA KWA UMMA
Mtandao wa habari za michezo wa www.sokakiganjani.blogspot.com unapenda kuwashukuru wadau na wasomaji wetu wote kwa ushirikinao mkubwa na uaminifu ambao mmekuwa mkitupatia. Hatukupenda kusitisha huduma zetu bali pia hatukupenda kukwaruzana na TCRA kutokana na masharti ambayo hatuwezi kuyamudu/kutimiza tunasitisha huduma zetu kwa muda usiojulikana kuanzia leo tarehe 15 juni 2018.

By Alexander Victor:
Blogger @ sokakiganjani.blogspot.com
follow us on facebook: @ vyankende.com, twitter: @vyankendeVictor, Instagram: @vyankendesports
+255 656 800 588

Jerry Muro Amwaga Kinachoiangamiza Yanga.


Afisa Habari wa zamani katika klabu ya Yanga, Jerry Muro, amefunguka na kueleza kuwa suala la uongozi wa timu hiyo kumuondoa aliyekuwa kocha wake, Mholanzi, Hans van der Plujim kimizengwe ndiyo limeifikisha Yanga hapo ilipo.

Muro ameeleza kuwa dhambi na zinawatafuna viongozi wa Yanga waliopo madarakani hivi sasa akisema ndiyo wamesababisha timu kuyumba.

Mbali na hayo, Muro amesema yupo tayari kuchukiwa na wadau wa Yanga akiona ni vema auseme ukweli kwa kuibua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakifanyika ndani ya klabu.

Hatu hiyo imekuja kufuatia Yanga kuyumba kiuchumi na baadhi ya wachezaji wakihusishwa kuhama kuelekea mahala pengine kutokana na klabu kukumbukwa na hali ngumu kifedha.

"Ndugu zangu wa Yanga Sc niseme wazi hata kama mtanichukia ni heri nichukiwe Kwa kusema ukweli, kuna mambo mengine yanakwenda kwa laana, Kuna dhambi ambayo inawatafuna na itawatafuna sana hata akisajiliwa Cristiano Ronaldo Bado itawatesa sana"

"Kitendo cha kinyama na kihuni mlichomfanyia Babu Hans head coach wa Yanga Sc Kwa kumuondoa kwa mizengwe nasema wazi hapa hiyo laana itawatesa sana, nasema haya kwa kuwa nilikuwa najua kinachofanywa lakini sikuwa na uwezo wa kuzuia kisitokee ila iko siku nitawataja wote waliohusika na kuivuruga Yanga na kuifanya kufika ilipofika"

"Kuna Laana wanapata viongozi ambao leo wote hawako salama kuanzia mwenyekiti mpaka makamu Mwenyekiti na wengine ni shauri ya chuki, roho mbaya waliyomfanyia Babu Hans, Tazameni maisha yao binafsi kila mmoja anapambana na jambo lake kwa wakati wake iko siku nitasema tena kwa kishindo tu, Hii laana mtajuta wanasababisha mamilioni ya mashabiki wa Yanga wanakosa raha kwa Ushenzi wa wachache."

NASEMA TABUNI TENA TABUNI.

Ameandika Jerry Murro 

Aliyewahi kuwa Afisa habari wa klabu ya Yanga

Kombe La Dunia Kuanza Kutimua Vumbi Leo.


Leo Alhamisi June 14 Kivumbi cha kombe la Duni kinatarajiwa kuanza kutimuka kwa wenyeji kuwakalibisha Saudi Arabia katika pambano la ufunguzi.

RATIBA KAMILI WIKI HII.
18:00 Urusi vs Saudi Arabia

Kesho Ijumaa June 15
15:00 Misri vs Uruguay
18:00 Morocco vs Iran
21:00 Ureno vs Hispania

Jumamosi June 16
13:00 Ufaransa vs Australia
16:00 Argentina vs Iceland
19:00 Peru vs Dermark
22:00 Croatia vs Nigeria

Jumapili June 17
15:00 Costa Rica va Serbia
18:00 Ujerumani vs Mexico
21:00 Brazil vs Uswisi

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA RUSSIA 2018

Kundi A
1-Urusi
2-Saudi Arabia
3-Misri
4-Uruguay

Kundi B
1-Ureno
2-Hispania
3-Morocco
4-Iran

Kundi C
1-Ufaransa
2-Australia
3-Peru
4-Denmark

Kundi D
1-Argentina
2-Iceland
3-Croatia
4-Nigeria

Kundi E
1-Brazil
2-Uswisi
3-Costa Rica
4-Serbia

Kundi F
1-Ujerumani
2-Mexico
3-Sweden
4-Korea Kusini

Kundi G
1-Ubelgiji
2-Panama
3-Tunisia
4-England

Kundi H
1-Poland
2-Senegal
3-Colombia
4-Japan 

Simba Waanza Mazungumzo Na Wakal Wa Nyota Huyu.


Huyu anaitwa kiungo Mestro au rasta wa Gor Mahia, Francis Kahata Nyambura alizaliwa Ruiru Kenya may 04, 1992 ana umri wa miaka 26

Tayari klabu ya Simba Sc imeanza mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo ili aweze kujiunga na timu hiyo. Kahata ambaye anacheza namba 8 au 10 amewavutia Simba kwenye michuano ya kombe la Sportpesa Super Cup iliyomalizika hivi karibuni.

Kocha wa Simba, Masoud Djuma tayari aliwasilisha jina la Kahata  kwa mabosi wa klabu hiyo baada ya kuisha kwa michuano ya Sportpesa Super Cup.

@yossima Sitta Jr.

Magazeti Ya Michezo Tu Ya Tanzania Leo Alhamisi 14. 06.2018

Magazeti Ya Michezo Tu Ya Tanzania Leo Alhamisi Juni 14.2018
Amka Na Tetesi Za Usajili Ndani Ya Klabu Ya Yanga Leo Alhamisi Juni 24


Imebainika mlinda mlango wa Singida United Manyika Jr ameamua kuachana na klabu yake hiyo baada ya kutokea sintofahamu  baadhi ya malipo yake, Manyika ameamua aondoke rasmi kikosini humo na huenda akatua Yanga.

pia Yanga wanahusishwa kuitaka huduma ya aliyewahi kuwa kipa wao Deogratius Munishi Dida  ambaye kwasasa anakipiga south africa

Aitha Taarifa zinaeleza kua Fransis Kahata na Meddie Kagere wote toka gormahia wamo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Yanga.

Kagere tayari amebakiza mkataba wa mwaka mmoja gormahia pia Yanga na Gormahia wameingia kwenye vita ya kumuwania Laudit Mavugo kwa msimu ujao

Pascal wawa na Juma Nyoso nao wanatajwa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa VPL

LECHANTRE ASEPA KIROHO SAFI SIMBA SC.-Klabu ya Simba imeachana Rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Mfaransa Pierre Lechantre na kocha wa viungo Mohamed Aymen raia wa Tunisia baada ya mikataba yao ya miezi sita kuisha ndani ya klabu hiyo.

-Lechantre alikutana na uongozi wa klabu Simba jana jumanne kuhusu mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ila kwa masharti ambayo viongozi wa klabu ya Simba waliyaweka kocha Pierre hakuweza kukubaliana nayo.

-Kwa mjibu wa Pierre ambaye ameondoka  alfajiri ya leo kurudi kwao Ufaransa amedai Kuna mambo muhimu ambayo walishidwa kufikia makubaliano katika kusaini mkataba mpya na klabu ya Simba.

-Pierre ambaye ameisaidia klabu ya Simba kubeba ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara (vpl) kwenye usiku wa tuzo za Mo Simba Awards 2018 aliwashukuru Viongozi, wachezaji, wanachama wa klabu ya Simba na kuwatakia kila kheri

-Inasemekana Pierre Lechantre alikuwa anataka kuongezewa mkataba wa miaka mitatu na mshahara na pia alikuwa ameweka pendekezo la kutofanya kazi na kocha msaidizi wa klabu hiyo Masoud Djuma. Huku simba wao walitaka kumubadilishia cheo kuwa mkurungezi wa ufundi wa klabu hiyo na mshahara wa milioni 30 aliokuwa analipwa aupunguze uwe milioni 18 kitu ambacho Lechantre amekigomea.

-Pierre ameiongoza klabu ya Simba katika michezo 20 huku michezo 15 ya ligi kuu Tanzania Bara michezo 4 ya kombe la shirikisho Afrika na mchezo mmoja kwenye Sportpesa Super Cup.

-Katika michezo hiyo wameshinda michezo 13 ikiwa michezo 11 ya vpl na michezo 2 ya Kombe la shirikisho ametoa sare michezo 6 ikiwa michezo 3 ya Vpl, michezo ya 2 ya kombe la shirikisho na mmoja wa sportpesa na kufungwa mchezo 1 wa vpl.

Yanga, Simba at war over Kagere


Simba club's leadership through Information Officer, Haji Manara, said you are currently planning to register an international striker for an increase in the edge of the attack. 

Despite the presence of Emmanuel Okwi and John Bocco who were part of the Lion's contribution in the past season, the team's team still needs another striker. 

Manara has said that the current technical team is looking for who is to be registered and unable to openly expect to find a player from what nation.

The move immediately after the squad failed to win the net in the SportPesa championship that ended in the last few days in Kenya although its dependent attackers did not exist.


The registration will be the third of Simba after the end of the league where it has already merged three Marcel Kaheza, Adam Salamba and Mohamed Rashid.

 In addition, if Simba will be able to bring the player back, they will be responding to Yanga's strike, which starts the move against Meddie Kagere, who plays for Gor Mahia FC in Kenya

Villarreal Signs Striker Gerard Moreno from Espanyol


Spanish club Villarreal has signed striker Gerard Moreno from Espanyol.

Villarreal says Tuesday that Moreno has agreed to a five-year contract.

Villarreal already owned 50 per cent of the rights to Moreno, who had previously played for the club.

Espanyol says Villarreal bought the player’s full rights by paying 20 million euros (23.5 million dollars), which was half of his buyout clause.

The 26-year-old Moreno scored 39 goals in three seasons with Espanyol.

Villarreal finished the Spanish league in fifth place last season, earning it a berth to the Europa League.

Official release: Julen Lopetegui will coach Real Madrid after the 2018 World Cup in Russia


Julen Lopetegui will be the coach of Real Madrid after the 2018 World Cup in Russia.

Real Madrid CF announces that Julen Lopetegui will coach the first team for the next three seasons.

Julen Lopetegui will join the club after the participation of the Spanish team in the World Cup, after two years leading the national team

Ikirangamisi c’inkino z’igikombe c’isi yose zimirije.


Kuva kuri uyu wa kane igenekerezo rya 14 Ruheshi umwaka wa 2018 mu gihugu c’uburusiya igikombe c’isi yose kizoba gitanguye icese.
Iki niko kirangamisi:
Igenekerezo rya 14/06/2018
– Isaha 17h00 : Rusie Vs Arabie Saoudite
Igenekerezo rya 15/06/2018
-Isaha 14h00 : Egypte Vs Uruguay
– Isaha 17h00: Maroc Va Iran
– Isaha 20h00: Portugal Vs Espagne
Igenekerezo rya 16/06/2018
– Isaha 12h00: France Vs Australia
– Isaha 15h00 : Argentine Vs Island
– Isaha 18h00 : Perou Vs Danemark
– Isaha 21h00 : Croatie Va Nigeria
Igenekerezo rya 17/06/2018
– Isaha 14h00: Costa Rica Vs Rerbie
– Isaha 17h00 : Allemagne Mexique
– Isaha 20h00: Bresil Vs Suisse
Igenekerezo rya 18/06/2018
– Isaha 14h00: Suède Vs Corée du Sud
– Isaha 17h00 : Belgique Vs Panama
– Isaha 20h00: Tunisie Vs Angleterre
Igenekerezo rya 19/06/2018
– Isaha 14h00 : Colombie Vs Japon
– Isaha 17h00: Pologne Vs Senegal
– Isaha 20h00: Russie Vs Egypte
Igenekerezo rya 20/06/2018
– Isaha 14h00: Portugal Vs Maroc
– Isaha 17h00: Uruguay Vs Arabie Saoudite
– Isaha 20h00: Iran Vs Espagne
Igenekerezo rya 21/06/2018
– Isaha 14h00: Danemark Vs Australie
– Isaha 17h00: Francs Vs Perou
– Isaha 20h: Argentune Vs Croatie
Igenekerezo rya 22/06/2018
– Isaha 14h00 : Bresil Vs Costa Rica
– Isaha 17h00: Nigeria Vs Islande
– Isaha 20h: Serbir Vs Suisse
– Igenekerezo rya 23/06/2018
– Isaha 14h00: Belgique Vs Tunisie
– Isaha 17h00: Coree du Sud Vs Mexique
– Isaha 20h00: Allemagne Vs Suède
Igenekerezo rya 24/06/2018
– Angketerre Vs Panama
– Isaha 17h00: Japon Vs Senegal
– Isaha 20h00: Pologne Vs Colombie
Igenekerezo rya 25/06/2018
– Isaha 16h00: Arabie Saoudite Vs Egypte
– isaha 16h00: Uruguay Vs Russie
– Isaha 20h00: Espagne Vs Maroc
– Isaha 20h00: Iran Vs Portugal
Igenekerezo rya 26/06/2018
– Isaha 16h00: Danemark Vs France
– Isaha 16h00: Australie Vs Perou
– Isaha 20h00: Islande Vs Croatie
– isaha 20h00: Nigeria Vs Argentine
Igenekerezo rya 27/06/2018
– Isaha 16h00:Mexique Vs Suède
– Isaha 16h00: Coree du Sud vs Allemagne
– Isaha 20h00: Serbie Vs Bresil
– Isaha 20h00: Suicce Vs Costa Rica.

Kombe la dunia: Teknolojia ya VAR kuanza kutumiwa


Kombe la dunia nchini Urusi, litashuhudia matumizi ya kwanza ya teknolojia ya Video Assistant Referee, mfumo wa video unaomwezesha mwamuzi kupitia ,kwa kutezama matukio mbalimbali yanayotokea uwanjani, wakati mechi ikiendelea.
Shirikisho la soka duniani FIFA, limesema lengo la teknolojia hii ambayo tayari imeshafanyiwa majaribio hasa katika ligi za soka barani Ulaya, itasaidia kuleta ukweli na haki katika michuano hii.
Teknolojia hii itafanya vipi kazi ?
Jambo la kwanza ni kuwa teknolojia hii ya VAR, itatumiwa katika mechi zote 64 za kombe la dunia, kwa lengo la kutatua yafuatayo:-
-Kubaini iwapo goli limeingia na namna lilivyofungwa.
-Uamuzi wa kutoa mkwaju wa penalti, na sababu zilizosababisha hali hiyo kutokea.
-Iwapo mchezaji anastahili kupewa kadi nyekundu.
-Kuthibitisha jambo muhimu wakati wa mchezo huo.
Mwamuzi wa Kati kwa ushirikiano na maafisa wengine, watawasiliana ili kwenda kuthibitisha tukio fulani kupitia runinga, zitazokuwa zimetengwa katika eneo husika ili kurahihisha suala hili.

Waamuzi kutoka Afrika watakaochezesha kombe la dunia


Waamuzi sita kutoka barani Afrika, ni miongoni mwa Waamuzi 36 wa Kati, watakaochezesha miaka ya kombe la dunia nchini Urusi kuanzia wiki hii.
Miongoni mwa Waamuzi hao ni pamoja na Abid Charef Mehdi kutoka Algeria.
Wengine ni pamoja na Diedhiuou Malang kutoka Senegal, Gassama Bakary Papa kutoka Gambia, Grisha Ghead raia wa Misri, Sikazwe Janny wa Zambia na Tessema Weyesa Bamlak raia wa Ethiopia.
Said Belqola raia wa Morocco, alikuwa mwafrika wa kwanza kuchezesha fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 kati ya Brazil na Ufaransa.
Belqola alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 45, baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.
Mashindano ya mwaka huu pia yana waamuzi wengine wasaidizi 63 huku bara la Afrika likiwakilishwa na waamuzi tisa.
Waamuzi wasaidizi hao ni pamoja na Achik Redouane (Morocco), Ahmed Waleed (Sudan) Birumushahu Jean Claude (Burundi), Camara Djibril (Senegal), Dos Santos Jerson Emiliano (Angola), Etchiali Abdelhak (Algeria), Hmila Anouar (Tunisia), Samba El Hadji Malick (Senegal) na Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini).

Azama Yamnasa Kocha Wa Yanga.


Aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu za Yanga na Mbeya city, Juma Mwambusi amejiunga na klabu ya Azam kama kocha msaidizi wa klabu hiyo. Mwambusi amesaini kandarasi ya miaka miwili na kuungana na kocha mkuu Hans Van der Pluijm ndani ya Azam Fc.

Azam FC yanasa saini ya Nchimbi

Ditram Nchimbi Azam
Ditram Nchimbi Azam


KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imethibitisha kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji Ditram Nchimbi, akitokea Njombe Mji.

Nchimbi ni mmoja ya washambuliaji wachache kwenye ligi ambao wanatambulika kwa uwezo wa kupambana na mabeki kwa mipira ya juu na chini, akitarajiwa kuongeza kitu katika eneo la ushambuliaji la Azam FC.

Zoezi la uingiaji mkataba baina ya pande hizo mbili limesimamiwa na Meneja wa timu hiyo, Phillip Alando, ambaye ameweka wazi kuwa ujio wa mshambuliaji huyo ni katika kuboresha eneo la ushambuliaji.

Mshambuliaji huyo aliyeipandisha Majimaji miaka mitatu iliyopita kwa mabao yake 10, amewahi pia kuichezea Mbeya City, ataanza kuonekana rasmi Azam FC kuanzia msimu ujao wakati timu hiyo ikianza kutetea ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kutimua vumbi kuanzia Juni 29 hadi Julai 13 mwaka huu.

Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC kuelekea msimu ujao, awali ikitangulia kuwasajili nyota wawili kutoka Zimbabwe mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Tafadzwa Kutinyu, wote wakipendekezwa na Kocha Mkuu mpya, Hans Van Der Pluijm

Usajili Ulio Kamilika Singida United Msimu Huu.

singida united
Singida United Logo

Klabu ya Singida United ambao wamemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Sportpesa iliyomalizika jumapili iliyopita june 10. Tayari Singida imekamilisha usajili wa wachezaji Tibar George kutoka Ndanda Fc, Habib Kiyombo kutoka Mbao Fc, Diaby Amara kutoka Asec ya Ivory Coast, Feisali Salum kutoka JKU ingawa bado hawajamtambulisha rasmi.

Pia klabu hiyo imemrejesha kundini beki wao wa kimataifa wa Zimbabwe, Elisha Muroiwa ambaye aliondoka Singida mwezi December mwaka jana kwa Sababu ya matatizo ya kifamilia pia Danny Lyanga atakuwa huru kuitumikia klabu ya Singida msimu ujao baada ya adhabu yake ya miezi sita kuisha huku Mbrazili Felipe Santos bado hajasaini mkataba.


Baada ya usajili huo klabu ya Singida United itaachana na wachezaji wafuatao kwa sababu mbalimbali Tafadzwa Kutinyu ameondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Azam Fc. Mudathir Yahya mkataba wake umeisha na klabu ya Singida United kwa sasa ni mchezaji huru.

Danny Usengimana na Michael Rusheshagonga wote raia wa Rwanda wataachana na klabu hiyo kutokana sababu inayotajwa klabu ya Singida United kushindwa kutimiza matakwa ya kimkataba Danny Usengimana alisajiliwa kwa dau la milioni 200 ila amelipwa milioni 80 tu na zingine hajalipwa mpaka sasa hivyo hivyo kwa Rusheshagonga.

Papy Kambale yeye anaachwa kwa sababu ya kufanya utovu wa nidhamu kila mara ndani ya klabu hiyo. Shafik Batambuze anaachana na Singida United kwa sababu kutotimiziwa matakwa ya kimkataba huku Deus Kaseke akitarajiwa kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini ila akifeli anaweza akajiunga na Azam moja kwa moja.

WASHINDI WA TUZO ZA MO SIMBA AWARDS 2018


👉Tuzo ya Benchi la Ufundi imekwenda kwa MaKocha
Pierre Lechantre Masoud Djuma
Mohammed Aymen benchi zima la ufundi la klabu hiyo .

👉Goli bora la mwaka la Simba SC  mshindi n John Bocco  ,goli alilofunga katika  mchezo dhidi ya Mwadui FC .

👉Mchezaji Bora chipukizi  wa klabu ya Simba SC Rashidi Juma

👉Mshambuliaji  bora wa mwaka wa Mo Simba Awards 2018 ni Emmanueli  Okwi bora

👉Kiungo Bora wa Mwaka Simba SC  Tuzo imekwenda kwa  Shiza Ramadhani Kichuya

👉Erasto Nyoni  ameshinda tuzo ya Beki  bora wa mwaka wa klabu ya soka ya simba .

👉Kipa Bora wa Mwaka klabu ya  SimbaSC ni Aishi Manula

👉Mhamasishaji bora wa mwaka Simba SC ni Haji Manara

👉Tuzo ya Mhamasishaji bora wa mwaka kwenye mitandao ya kijamii imekwenda kwa Mwana FA na Salama Jabiri.

👉Tuzo ya Shabiki bora wa mwaka imekwenda kwa Marehemu Bi Fihi Kambi RIP.

👉Tuzo ya Tawi bora la Mwaka Simba SC imekwenda katika tawi la  Ubungo Terminal.

👉Kiongozi bora wa Mwaka Simba SC tuzo imekwenda kwa Kaimu Rais wa  klabu ya Simba SC Salimu Abdallah 'Try Again

👉Mchezaji bora wa Mwaka Captain John Bocco.

👉Mchezaji bora wa kike Zainabu Rashidi

👉Tuzo ya Heshima imekwenda kwa mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Simba Suleiman Matola

👉Tuzo ya mchakato wa mabadiliko imekwenda kwa wote walio husika .

©Sokaplace2018

Kikosi Cha Simba Dhidi Ya Gormahia Kitakachocheza Fainali Ya SportPesa Super Cup1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Yusuf Mlipili
4. Paul Bukaba
5. Erasto Nyoni
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yassin
9. Mohammed Rashid
10. Rashid Juma
11. Adam Salamba

AKIBA:
Ally Salim
Shomari Ally
Mohammed Hussein
Marcel Kaheza
Moses Kitandu

Taarifa Kutoka Azam Kuhusu Jeraha La Ngoma


Daktari wa timu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa amethibitisha kuwa mshambuliaji Donald Ngoma atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tisa.

Dokta Mwankemwa amerejea leo saa tatu asubuhi kutoka Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya St. Vincent Parrot.

Mwankemwa amesema Ngoma alikuwa ana uvimbe kwenye goti la kulia ambapo baada ya vipimo imeonekana alikuwa amechanika kidogo japo tayari ameanza kupona.

Hata hivyo dokta huyo aliongeza kuwa Ngoma hatafanyiwa upasuaji badala yake ataendelea kufanya mazoezi mepesi ya kawaida mwenyewe kabla ya kupona kabisa na kurejea uwanjani.

"Vipimo alivyofanyiwa Ngoma vinaonyesha atakaa nje ya uwanja kwa wiki tisa ili kupona kabisa ambapo itakuwa hadi mwezi wa Agosti," alisema Dk. Mwankemwa

Kauli Ya Kocha Masoud Djuma Kuelekea Mchezo Wa Kesho


Kaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya Gor Mahia watacheza tofauti na watu walivyozoea.

Katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, Simba haikuwa kwenye kiwango bora sana kitu ambacho kocha Masoud ameahidi kutotokea kesho.

Masoud amesema ingawa hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kuliko wapinzani wao Gor lakini wamejipanga kufanya maajabu na kurejea na kombe nyumbani.

Raia huyo wa Burundi ameongeza kuwa siku zote mchezo wa fainali unakuwa wa tofauti na amewaandaa wachezaji wake vizuri na watu wategemee mchezo wa tofauti kesho.

"Kesho tutaingia kivingine kabisa kuliko tulivyocheza mechi zilizopita, wenzetu wefunga mabao matano sisi hatujafunga hata moja lakini kesho tutafanya hivyo.

Mungu ndio anajua nani atachukua ubingwa lakini sisi tutapambana mpaka tone la mwisho," alisema Masoud.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiriKaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya Gor Mahia watacheza tofauti na watu walivyozoea.

Katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, Simba haikuwa kwenye kiwango bora sana kitu ambacho kocha Masoud ameahidi kutotokea kesho.

Masoud amesema ingawa hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kuliko wapinzani wao Gor lakini wamejipanga kufanya maajabu na kurejea na kombe nyumbani.

Raia huyo wa Burundi ameongeza kuwa siku zote mchezo wa fainali unakuwa wa tofauti na amewaandaa wachezaji wake vizuri na watu wategemee mchezo wa tofauti kesho.

"Kesho tutaingia kivingine kabisa kuliko tulivyocheza mechi zilizopita, wenzetu wefunga mabao matano sisi hatujafunga hata moja lakini kesho tutafanya hivyo.

Mungu ndio anajua nani atachukua ubingwa lakini sisi tutapambana mpaka tone la mwisho," alisema Masoud.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiri

Team Samata Yainyuka Team Kiba


Team Samata imeinyuka Team Alikiba kwa jumla ya goli 4-2 katika mchezo wa kirafiki.
FT Team Samata 4-2 Team Alikiba
  Mohamed Samata     Ibrahim Ajibu
 Jamhuri Jr                   Ibrahim Ajibu
 Haruna Moshi Boban
 Mbwana Samatta


Powered by Blogger.

Total Pageviews

Popular Posts

Recent Posts

3/recent/post-list

Random Posts

3/random/post-list
Soccer Transfer News
recent/hot-posts