Ngorongoro Heroes wawaponda kichwa koboko wa Msumbiji



Timu ya soka ya Taifa kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Timu ya vijana ya Msumbiji katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo timu ya vijana wa Msumbiji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 13 kwa njia ya penati iliyochongwa na Leonel Victor baada ya kipa wa Ngorongoro Hereos Aboutnalib Mshery.
Baada ya bao hilo vijana wa Ngorongoro Heroes waliamka na kuanza kucheza kandanda la pasi zaidi ambapo kwa staili walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Abdul Hamis Suleiman katika dakika ya 35.
Dakika ya 59 Ngorongoro Heroes walipata penati baada ya mchezaji wao kuangushwa ndani ya 18 lakini Hasadi Ally Juma alishindwa kuukwamisha mpira huo wavuni na kuishia mikononi mwa kipa Julio Matevel.
Aidha Mwamuzi wa mchezo huo Erick Onoka kutoka Mwanza alimuonesha kadi nyekundu nahodha wa Msumbiji Marithno Albetro baada ya kumchezea madhambi kiungo wa Ngorongoro Heroes Kelvin Nashon.
Ngorongoro Heroes walipata bao la pili katika dakika ya 71 kupitia kwa kijana wa timu ya Yanga Said Mussa Bakari baada kurudishia mpira wa faulo uliopanguliwa na kipa wa Msumbuji Julio Matevel.
Ushindi wa pili
Hiyo inakuwa ni mechi ya pili kwa Ngorongoro Heroes kupata ushindi katika mechi zake za kirafiki baada ya Jumapili iliyopita kuwafunga Morocco kwa bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na Muhsin Makame, mchezo ambao ulifanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mechi hizo ni kwa ajili ya maandalizi kuelekea mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger ambapo Tanzania wamepangwa kuumana na DR Congo katika mechi ya awali.
Mechi ya kwanza itafanyika Machi 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadae mjini Kinshasa ambapo mshindi katika mechi hiyo atakutana na Mali katika hatua inayofuata.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.