Njombe Mji Kumtuliza Simba Mwenye Hasira Kali.
KOCHA Msaidizi wa timu ya Njombe Mji, Mrage Kabange, amesema wanajipanga vilivyo ili kukwepa kipigo
kutoka kwa Simba ambao wana hasira
ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wekundu hao wa msimbazi waliondoshwa kwenye michuano hiyo
na timu ya Al Masry ya nchini Misri ambayo imevuka kutokana na
faida ya mabao mawili waliyoyapata ugenini katika mechi ya awali iliyoisha kwa sare ya 2-2.
Simba na Al Masry walitoka sare ya 2-2
katika mechi ya awali ya hatua ya 32 bora iliyochezwa Machi 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na waliporudiana walitoka suluhu.
Njombe Mji wanatarajia kuikaribisha
Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.
Akizungumzia mchezo huo Kabange
alisema kutokana na matokeo hayo, anaamini Simba itahitaji ushindi
ili kuwapoza mashabiki wake kwa kutolewa kwenye michuano ya
kimataifa, lakini wao wamejiandaa vilivyo kukabiliana nao.
Alisema mchezo utakuwa mgumu
kwao kutokana na wapinzani wao kuwa na Kikosi kipana chenye
wachezaji mahiri, lakini watajipanga
sawasawa na kama itatokea kufungwa, basi hawatakubali kuruhusu
mabao mengi.
“Tunajua wapinzani
wetu watakuwa na
hasira ya kuondolewa
kwenye Kombe la
Shirikisho Afrika, hivyo
hasira zao watazielekeza
Ligi Kuu, sisi tutapamba
kadiri ya uwezo wetu
na hatuwezi kukubali
kufungwa ovyo,” alisema
Kabange.
Hata hivyo, Kabange aliwataka wachezaji wake kuongeza bidii
na kufuata maelekezo wanayopewa kwani umakini ni muhimu katika mchezo huo.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.