LECHANTRE ASEPA KIROHO SAFI SIMBA SC.



-Klabu ya Simba imeachana Rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Mfaransa Pierre Lechantre na kocha wa viungo Mohamed Aymen raia wa Tunisia baada ya mikataba yao ya miezi sita kuisha ndani ya klabu hiyo.

-Lechantre alikutana na uongozi wa klabu Simba jana jumanne kuhusu mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ila kwa masharti ambayo viongozi wa klabu ya Simba waliyaweka kocha Pierre hakuweza kukubaliana nayo.

-Kwa mjibu wa Pierre ambaye ameondoka  alfajiri ya leo kurudi kwao Ufaransa amedai Kuna mambo muhimu ambayo walishidwa kufikia makubaliano katika kusaini mkataba mpya na klabu ya Simba.

-Pierre ambaye ameisaidia klabu ya Simba kubeba ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara (vpl) kwenye usiku wa tuzo za Mo Simba Awards 2018 aliwashukuru Viongozi, wachezaji, wanachama wa klabu ya Simba na kuwatakia kila kheri

-Inasemekana Pierre Lechantre alikuwa anataka kuongezewa mkataba wa miaka mitatu na mshahara na pia alikuwa ameweka pendekezo la kutofanya kazi na kocha msaidizi wa klabu hiyo Masoud Djuma. Huku simba wao walitaka kumubadilishia cheo kuwa mkurungezi wa ufundi wa klabu hiyo na mshahara wa milioni 30 aliokuwa analipwa aupunguze uwe milioni 18 kitu ambacho Lechantre amekigomea.

-Pierre ameiongoza klabu ya Simba katika michezo 20 huku michezo 15 ya ligi kuu Tanzania Bara michezo 4 ya kombe la shirikisho Afrika na mchezo mmoja kwenye Sportpesa Super Cup.

-Katika michezo hiyo wameshinda michezo 13 ikiwa michezo 11 ya vpl na michezo 2 ya Kombe la shirikisho ametoa sare michezo 6 ikiwa michezo 3 ya Vpl, michezo ya 2 ya kombe la shirikisho na mmoja wa sportpesa na kufungwa mchezo 1 wa vpl.