Amka Na Taarifa Hizi Kutoka Yanga Leo March 20


Mara baada ya kurejea nchini kukokea Botswana uongozi wa klabu ya Yanga leo  unatarajiwa kufanya Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo majra ya saa nane mchana.

Kesho Ndio Kesho.

Ile droo ya mtoano kusaka timu 16 zitakazotinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika itafanyika kesho huku klabu ya Yanga ambayo pia ilitupwa kunako kombe la Shirikisho ikitokea klabu bingwa itakuwa kikaangoni..

Droo hiyo itahusisha timu 16 zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa na 16 zilizofuzu kwenye raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho.

Yanga ya Tanzania ni miongoni mwa timu zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa hivyo itapangiwa mpinzani wake kutoka miongoni mwa lizizofuzu raundi ya kwanza kombe la Shirikisho.

Hizi hapa timu za mtoano



Michezo ya mtoano kwa ajili ya makundi ya kombe la Shirikisho itapigwa kati ya April 06-08 huku ya marudio ikitarajiwa kupigwa siku 10 baadae.

Timu kutoka ligi ya mabingwa zitaanzia nyumbani.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.