Samatta Atua Algeria Kuungana Na Timu Ya Taifa


Nahodha  wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta tayari wamewasili nchini Algeria akitokea Ubeligiji anakochezea kunako klabu ya Genk.

Samatta ametua Algeria ili kuungana na wachezaji wenzake 20 wa kikosi hicho ambao wataliwakilisha taifa kwenye michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa mmoja ukiwa ni dhidi ya Algeria na mwingine dhidi ya Dr Congo.

Pichani ni Mh Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuf Mzee akimpokea Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta alipowasili jioni ya leo Uwanja wa Ndege wa Algiers tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa Algeria vs Tanzania utakaochezwa Machi 22,2018 uwanja wa 5 July jijini Algiers.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.