Kocha Simba Kuiangamiza Yanga Kwa Mbinu Hii.
Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, anaamini amepata mbinu ya kuwashughulia Yanga katika mchezo wa ligi dhidi yao utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Aprili 29 2018.
Mfaransa huyo alihudhuria mechi ya Yanga dhidi ya Singida United iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii ili kuwasoma watani wake.
Baada ya mchezo huo, Lechantre alisema kuwa kuna baadhi ya wachezaji aliokuwa akiwatazama vizuri hivyo atahakikisha anawashugulikia vizuri.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Lechantre alionekana Uwanjani akiwa na notebook akiandika baadhi ya vitu wakati mchezo huo ukiwa unaendelea.
Yanga hivi sasa ipo katika maandalizi ya safari kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha na Simba wanajiandaa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.