Mexime: Iwe Kinyumenyume Ama Kimbelembele, Tutapambana
Kocha mkuu wa klabu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema klabu yake leo itapambana kwa hali na mali kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wa ligi dhidi ya mwadui fc
Akihojiwa na Chombo cha Habari, EFM Radio, Kocha wa Maxime, amesema wao wamejipanga na watajua namna gani ya kupata matokeo kwenye mchezo wa leo.
"Tunajua namna ipi tumejipanga, iwe kinyumenyume ama kimbelembele, tutapambana" alisema.
Kagera Sugar itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Kaitaba ikiikaribisha Mwadui FC, mechi ambayo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Kiwango cha Kagera msimu huu hakijawa kizuri kutokana na timu hiyo ipo kwenye harakati za kuepuka kushuka daraja.
Timu hiyo ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo ikiwa na pointi 18.
Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.