Amka na taarifa hii kutoka Simba sc leo jumapili September 2



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Bw Boniface Lyamwike leo Jumapili tarehe 2/9/2018 Saa Tano na nusu asubuhi itazungumza na Waandishi wa habari za michezo

Mkutano huo muhimu unalenga kuelezea maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Simba na utafanyika kwenye Ukumbi wa kivukoni One,uliopo ndani ya Hoteli ya Serena ya hapa jijini Dar es salaam.

IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SPORTS CLUB

SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.