Kiyombo mambo ni moto Afrika Kusini.
Baada ya kung’ara na klabu ya Mbao Fc mshambuliaji Matata Habib Kyombo alinaswa na mabwenyenye wa Singida United kwa mkataba wa miaka mitatu.
Msimu wake wa kwanza amepata bahati ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya majaribio.
“Habib Kyombo amempata mwaliko wa siku 10 kwenda kufanya majaribio ndani ya klabu ya Mamelod Sundowns” Msemaji wa Singida alithibitisha hilo
Habib Kyombo kwa sasa yupo Africa kusini kwa ajili ya majaribio hayo. Klabu yake ya sasa Singida imesema ipo tayari kumruhusu mchezaji huyo kubakia afrika kusini kama atafanikiwa kubakia huko.
“Tumtakia baraka zote Habib. Tupo tayari kumruhusu kubaki klabuni hapo maana akifanikiwa yeye na sisi Singida tumefanikiwa” Alisema Festo Sanga
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.