Yanga Yamejirudia Yaleyale Ya Miaka Mitano Nyuma


 Mara ya mwisho Yanga kumaliza nafasi ya tatu Simba ilitwaa bingwa ni miaka tano iliyopita.

Katika msimu 2011/12, Yanga ilimaliza ya tatu Simba ikiwa bingwa na Azam ikishika nafasi ya pili.

Katika msimu huu Yanga ilikuwa na migogoro ya uongozi na katika mchezo wake wa mwisho ilifungwa na Simba mabao 5-0 na kusababisha aliyekuwa mwenyekiti wake Lyod Nchunga kujiuzuru.

Msimu huu Yanga imemaliza ya tatu ikiwa bila ya mwenyekiti wake Yusuf Manji aliyejiuzuru na mwenendo wa timu hiyo umekuwa wa kusuasua na mechi yake ya mwisho jana ilifungwa mabao 3-1 na Azam kwenye Uwanja wa Taifa.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa kuwathiri mabingwa hao wa kihistoria nchini mpaka kumaliza nafasi ya tatu ni kuandamwa na majeraha kwa wachezaji wao muhimu.

Ndani ya misimu yote miwili, 2017/18 na 2011/12 ambayo Yanga imemaliza kwenye nafasi ya tatu, Simba ndio waliotwaa ubingwa wa ligi hiyo huku Azam wakimaliza kwenye nafasi ya pili.

Katika msimu mitano ambayo Yanga ilikuwa ikitesa, Ligi Kuu Tanzania Bara, imetwaa mataji ya ligi hiyo mara nne huku wakiweka rekodi ya kuchukua mara tatu mfululizo kwenye misimu ya 2014/15, 2015/16 na 2016/17.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.