Simba Na Yanga Kukutana Kabla Ya Fainali? Hii Hapa Ratiba Kamili Ya SportPesa Super Cup. 2017/2018
Simba na Yanga zinaweza kujikuta zinakutana mwaka huu kwa mara ya tatu mfulilizo lakini safari hii ikiwa ni katika michuano ya SportPesa Super Cup.
Michuano hiyo inafanyika jijini Nairobi, Kenya na itakutanisha timu nane kutoka Tanzania na nne za wenyeji Kenya.
Michuano ya SportPesa Super Cup inaanza Juni 3 hadi Juni 10 na Simba wataanza Sharks ya Kenya wakati Yanga baadaye watakuwa uwanjani dhidi ya Homeboyz.
Kama kila timu itashindana, uwezekano wa kukutana ni asilimia kubwa na kila mmoja atalazimija kujiweka vizuri mapema kabisa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.