Kambi Ya Yanga Imenoga Wawili Warejea Kuongeza Nguvu, Simba Mbona Shughuli Wanayo.


Kambi ya Yanga mkoani Morogoro inaendelea kunoga juzi wachezaji watatu Amis Tambwe, Ibrahim Ajibu na Andrew Vicent Dante waliokuwa majeruhi walirejea kujiunga na kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba Jumapili Apri 29.

Kama hiyo haitoshi jana jioni mshambuliaji wa klabu hiyo ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu Donald Ngoma amejiunga na kambi ya klabu hiyo mkoani Morogoro. Pia kiungo wa wa kimataifa wa Congo, Papy Tshishimbi naye amerejea na kujiunga na kambi ya klabu ya Yanga Mkoani Morogoro.

Papy aliumia kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa kombe la Caf Confederation Cup dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia na alikosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City. Pia mshambuliaji Obrey Chirwa yeye baada ya mechi dhidi ya Mbeya City alirejea Dar kwa matatizo ya kifamilia ila jana jioni amejiunga na kambi hiyo.

Pia Beki kisiki wa klabu hiyo Kelvin Yondani naye ameanza mazoezi na wenzake baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliofanyika jumapili iliyopita April 22. Docta wa klabu hiyo Edward Bavu amesema wachezaji wote waliopo kambini wako fiti limebaki jukumu la kocha tu.

Klabu ya Yanga ipo nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na Pointi 48 baada ya kucheza michezo 23 huku Simba wakiongoza ligi kwa kuwa na pointi 59 ikiwa imecheza michezo 25. Huku vinara kwenye ufungaji ni Emmanuel Okwi wa simba akiwa na magoli 19 akifuatiwa na John Bocco wa Simba akiwa na magoli 14 huku Obrey Chirwa akiwa nafasi ya 3 akiwa amefunga magoli 12.

Mchezo wa Simba dhidi ya Yanga unasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka Tanzania utachezwa siku ya Jumapili april 29 ikiwa viingilio ni elfu 7 kwa mzunguko, VIP B na C ni 20,000 huku VIP A ni 30,000 pia Kwa mjibu wa TFF mageti ya Uwanja wa Taifa yatafunguliwa saa2:00 asubuhi chakula na vinywaji vitakuwepo uwanjani

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.