Simba vs Yanga Mechi 5 Za Kihistoria, Imo Na Ile Ya goli 5-0 ambazo Yanga Walimfunga Simba.


Kuelekea mtanange wa kukata na shoka wa Derby ya Kariakoo una tarajiwa kupigwa jumapili hii mtandao wa sokakiganjani umeamua kukusogezea baadhi ya matukio muhimu yaliyowahi kujili kwenye mipambano ambayo imekuwa ikizikutanisha timu hizi.


Leo tunakusogezea mechi tano kali na za kihistoria ambazo zimewakutanisha vibopa hawa wa ligi kuu Tanzania Bara.



Yanga 5 - 0 Simba “Sunderland” (June 1, 1968)



June mosi mwaka 1968 ndipo historia yetu inaanzia wakati klabu ya Simba ikitumia jina la Sunderland ilikubari kipigo kitakatifu cha golo tano kwa mtungi 5-0 kutoka kwa Yanga.

Katika mchezo huo magoli yalipachikwa kambani na Saleh Zimbwe aliyefunga magoli 2, Maulid Dilunga naye magoli 2 huku goli la tano likipachikwa kambani na Kitwana Manara "Popat".


Na mchezo huu ulipigwa ikiwa ni miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa ligi ya Tanzania.

Simba 6 - 0 Yanga (July 19, 1977)



Akiwemo mzee wetu, mzee wa Soka, Abdallah Kibadeni "King" hapa Simba waliiadhibu Yanga kwa kipigo kitakatifua cha goli 6-0 huku "King" akiingia kambani mara tatu yaani hat trick.

Kibadeni alifunga magoli hayo mnamo dakika za 10, 42 na 89 wakati magoli mengine yakifungwa na Seleman Sanga na goli la kujifunga la Ezekiel Greyson “Jujuman”.


Msimu huo Simba ilitwaa Ubingwa wa ligi hiyo wakati ambapo Yanga walikuwa na misuguano ya ndani ya klabu.


Pambano hili huenda likaendelea kukumbukwa kwani ndilo pambano lenye rekodi ya kufungwa kwa hati trick katika mchezo wa watani wa jadi.


Yanga 0 v 5 Simba (May 7, 2012)



Mara baada ya mechi ya kihistoria ililyopigwa mwaka 1977 mechi nyingine ya watani hao iliyokuwa na matokeo makubwa ya timu kufungwa magoli mengi ni pambano hili la mwaka 2012 ambapo Simba ilifumua Yanga goli 5-0


Hapa Mganda Emmanuel Okwi alipachika magoli mawili huku mengine yakifungwa na Felix Sunzu, Juma Kaseja na Patrick Mafisango.


Simba 3 - 3 Yanga (October 20, 2013)



Katika mchezo huu yanga ilipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwani ilitamatisha kipindi cha kwanza ikiongoza mchezo kwa goli 3-0 kwa magoli ya Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza aliyefunga magoli mawili. 


Lakini mambo yalibadilika katika kipindi cha pili baada ya Simba kurejesha magoli yote na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 3-3, magoli ya Simba yakifungwa na Betram Mwombeki,George Owino na Gilbert Kaze.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.