BAADA YA SALAMBA SASA NI ZAMU YA TSHISHIMBI.



Kuanzia asubuhi ya leo kumeibuka tetesi zinazomhusisha kiungo wa kimataifa wa Congo anaichezea klabu ya Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi kutakiwa na mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara (vpl) msimu wa 2017/18 klabu ya Simba.

Tetesi hizo zinadai tayari Simba inamunyemelea kiungo huyo ili acheze msimbazi msimu ujao ila ukweli ni kwamba Papy Tshishimbi bado ana mkataba na klabu yake ya Yanga hivyo Tshishimbi kwenda Simba mpaka klabu ya Yanga ikubali kumuuza kiungo huyo.

Wachezaji wa klabu ya Yanga ambao wanamaliza mikataba yao msimu huu ni golikipa Benno Kakolany, Mabeki Juma Abdul, Hassan Kessy, Andrew Vicent Dante, Kelvin Yondani, Pato Ngonyani na Nadir Haroub Cannavaro viungo ni Said Juma Makapu, Emmanuel Martin, Geofrey Mwashiuya na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.