TAIFA STARS YAIFUATA ALGERIA, WANNE WAKICHOMOLEWA KIKOSINI.



Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimeondoka mchana wa leo kwenda nchini Algeria, huku wachezaji wanne wakiondolewa katika kikosi hicho kutokana na sababu za kiafya na majeruhi.

Wachezaji hao ni Farid Musa na Thomas Ulimwengu ambao wamekosa ruhusa kutoka kwenye timu zao, wakati John Bocco na Hamis Abdallah wakiondolewa kwa sababu za kiufundi.

Kocha mkuu Salum Mayanga na msaidizi wake Hemed Morocco wamewaongeza wachezaji wengine ambao ni Rashid Mandawa, Himid Mao na Shabaan Idd.

Wachezaji wa Simba waliotoka nchini Misri wataungana na wenzao nchini Algeria, pamoja na Mbwana Samata na Saimon Msuva.

Machi 22 saa 2:00 usiku, Taifa Stars itacheza na timu ya taifa ya Algeria ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa FIFA.

Machi 27, Taifa Stars itacheza mchezo wa pili dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.