TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JUMATATU MARCH 19.2018
Lionel Messi ameitaka Klabu yake kujaribu Kumsajili beki wa Chelsea Marcos Alonso,Messi Alivutiwa na kiwango cha Mhispania huyo wakati timu zao zilipokutana katika ligi ya Mabingwa Ulaya
Klabu ya Manchester City Imepanga kuwasajili Wachezaji wawili ifikapo Mwisho wa Msimu huu,Mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane na Kiungo wa Real Madrid Isco wote wanatakiwa na Pep Guardiola Katika Kikosi chake.
Borusia Dortimund ipo tayari kutoa €40M ili Kumsajili Mshambuliaji wa Klabu ya Racing Club Lautaro Martinez.
Kocha Mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameendelea Kusisitiza kuwa Mshambuliaji wake Gareth Bale ana furaha Klabuni hapo na ataendelea kuwepo kwa Miaka zaidi.
Everton wapo tayari kumpa ofa £8M Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere Ajiunge na timu hiyo atakapo maliza Mkataba wake na Klabu yake Mwishoni mwa msimu.
Real Madrid itamuachia Kiungo wa Luka Modric Kujiunga na Moja ya Vilabu Kutoka Uingereza vinavyowania saini yake ikiwa tu watampata Emre Can wa Liverpool kuziba nafasi yake.
Klabu ya Arsenal Imepanga Kumsajili Mshambuliaji wa AC Milan Andre Silva Mwezi Juni.
Liverpool na Arsenal zote zinahusishwa kutaka kumsajili golikipa wa Atletico Madrid Jan Oblak.
Imeripotiwa kuwa Manchester City ikishindwa Kumsajili Mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane basi itapambana na Barcelona kuwania saini ya Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann.
Liverpool ipo tayari kuishinda Real Madrid kwa kutoa £70M Kumsajili kipa wa Roma Allison pia Chelsea wapo katika mbio za kumtaka kipa huyo wa kibrazil.
Chelsea inahusishwa kutaka kuwasajili Wachezaji wawili Kutoka Napoli beki Koulidou Koulibaly na Mshambuliaji Dries Martens pia Manchester United inamtaka Mshambuliaji huyo.
Manchester United ipo tayari kupambana na Real Madrid kumsajili Mshambuliaji wa PSG Neymar Jr.
Kiungo wa Real Madrid Luka Modric ameitaka Klabu yake kuhakikisha inamsajili Kiungo wa Tottenham Dele Alli kuchukua nafasi yake klabuni hapo kabla ya yeye hajaondoka.
Barcelona inakaribia kutangaza kukamilisha Usajili wa beki wa Bayern Munich David Alaba kwa £70M.
Beki wa Manchester United Luke Shaw amepanga kuhiama Klabu hiyo baada ya kushinda falsafa za kocha wake José Mourinho.
Chelsea na Real Madrid zinakaribia kufikia makubaliano ya Mabadilishano ya Wachezaji Eden Hazard kwenda Real Madrid na Marco Asensio kwenda Chelsea.
Raisi wa Real Madrid Florentine Perez amesema kuwa bado hajaona mbadala Sahihi wa luka Modric katika timu yake.
Juventus ipo tayari kutoa dau la kipengele cha uhamisho wa Kiungo wa Sevilla Steven Nzonzi ifikapo Mwisho wa Msimu huu.
Tottenham Imepanga kuimarisha eneo lao la ulinzi kwa Kumsajili beki wa Swansea City Alfie Mawson.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.