Watano Waondolewa Huku Watatu Wakiongezwa Kikosi Cha Stars Kitakachocheza mechi Za Kirafiki Dhidi Ya Algeria na Congo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza upya kikosi cha timu ya taifa huku akiwaongeza baadhi ya nyota kwenye kikosi hicho, awali aliita kikosi chenye jumla ya wachezaji 23 lakini baadhi wamepunguzwa kutokana na sababu mbalimbali.
Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.
Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na Shaaban Idd.
Kikosi hicho kitaondoka hapa nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kirafiki utakaopigwa Mach 22 2018
Kikosi kamili hiki hapa.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.