Kagame Cup kurejea baada ya miaka mitatu



Michuano ya vilabu inayosimamiwa na Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Maarufu Kama CECAFA Kagame Cup inatarajiwa kurejea katikati ya Mwaka huu baada ya kusimama kwa takribani miaka mitatu.

Hiyo yote inatokana na CECAFA kupokea kiasi cha Dollar Milioni Moja kutoka shirikisho la soka Ulimwengu (FIFA) ili kufanikisha mashindano mbalimbali yakiwemo ya vijana chini ya umri wa 17 yatakayofanyika nchini Burundi, pamoja yale ya Wanawake na wanaume kwa nchi wanachama.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka katika uongozi wa CECAFA ni kuwa michuano hiyo itafanyika kati ya Juni 30 hadi Julai 14 mwaka huu.

Itafanyika Dar

Taarifa zimezidi kusema kuwa michuano hiyo ilipangwa kufanyika nchini Djibouti lakini Azam TV ambao ndio Wameingia mkataba kurusha matangazo ya moja kwa moja wameshauri kubadilishwa kutokana na sababu za kiusalama yatafanyika jijini Dar es Salaam.

Mara ya mwisho mashindano hayo yalifanyika nchini Tanzania na Timu ya soka ya Azam kunyakua ubingwa kwa kumchapa Gor Mahia kutoka Kenya kwa mabao 2-0 na hiyo ilikuwa ni mwaka 2015

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.