Yule Rais Wa Klabu Moja Ugiriki Alieingia na Bastola Uwanjani Afungiwa Miaka Mitatu Na Faini.


Rais wa klabu ya PAOK Salonika amefungiwa miaka mitatu baada ya kuingia uwanjani akiwa na bastola katika mechi ya ligi kuu ya Ugiriki dhidi ya AEK Athens.

Rais uyo wa PAOK amepigwa faini ya Pauni 87,000 na bodi ya ligi ya Ugiriki . PAOK wamepokonywa pointi tatu na kupigwa faini ya Pauni 53,000,  pia watacheza mechi zao tatu zijazo za nyumbani bila mashabiki na wataanza msimu ujao wakiwa na upungufu wa pointi -2

Wapinzani wao kwenye mbio za Ubingwa AEK wamezawadiwa alama tatu kutokana na kuharishwa mechi hiyo ambapo ilikuwa 0-0 pindi Savvidis alipoingia uwanjani.

Ligi itaendelea tena siku ya Jumamosi baada ya kusimamishwa machi 12.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.