Yanga Walia Na Ratiba Kubana...

Akizungumza na wanahabari afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema wako kwenye harakati za kuandika kwenda kwenye Shirikisho kuangalia kama kutakiwa na uwezekano wa kusogezwa mbele kwa mchezo mmoja wapo kutokana na ratiba kubana.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu VPL wamerejea usiku wa kuamkia leo wakitokea Ushelisheli ambako walikwenda kucheza mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya St. Louis.


Baada ya kurejea klabu hiyo inatazamia kuwa na mchezo wa Azam Sports federation cup dhidi ya Majimaji utakaopiga mjini Songea 25.02.2018.

Kisha timu hiyo itasafiri kuelekea mkoani Mtwara kuwavaa Ndanda fc tarehe 28 .02 kabla ya kusafiri tena na kuelekea Manungu Morogoro kuwavaa Mtibwa Sugar.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.