Jeshi La Mtibwa Laifungia Safari Buseresere fc
Mabingwa wa kombe la shirikisho mwaka 2000 Mtibwa Sugar, wameanza safari asubuhi ya leo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) utakaochezwa jijini Mwanza katika dimba la Nyamagana dhidi ya Buseresere.
Mtibwa Sugar inaelekea jijini humo kwa kazi moja tu ya kusaka ushindi ili kuweza kusonga mbele katika kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup).
Wachezaji waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili hii ya February,25 saa 8 mchana ni makipa Shaban Hassan Kado na Benedictor Tinocco.
Mabeki waliosafiri ni Rodgers Gabriel “Jigwa’, Salum Kupela Kanoni “mbavu kunesa”, Hassan Mganga, Dickson Daud Mbeikya, Kassian Ponera na Hussein Idd Hante.
Viungo waliosafiri ni Henry Joseph Shindika, Shaban Mussa Nditi, Issa Kajia Mwanga, Ally Yusuf Makarani, Mohamed Issa Juma na Hassan Dilunga.
Washambuliaji ni Stamil Mbonde, Ismail Aidan Mhesa, Salum Ramadhani Kihimbwa na Haruna Chanongo.
Kikosi cha wana tam tam kilifanikiwa kufika hatua ya 16 bora ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuwafunga Villa Squad 2-1 ya jijini Dar es salaam na baadae kuwafunga Maji maji rangers kutoka Lindi 2-1.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.