SIMBA WAMESHINDA ILA PRISONS NI 'TIMU NA NUSU'

SIMBA WAMESHINDA ILA PRISONS NI 'TIMU NA NUSU'


Nilikuwa nasikia tu 'One Mistake, One Goal' ila usiku wa Jumatano hii ndio nimeshuhudia ukweli wa kauli hii. Kosa walilofanya Prisons katika dakika ya pili ya mchezo wao dhidi ya Simba ndilo lililoamua matokeo ya mechi hiyo. Tofauti na hapo, Prisons ni 'Timu na Nusu'. .

Nimesikia mashabiki wengi wakiibeza Simba kuwa licha ya usajili mkubwa na kambi ya Uturuki, bado wameambulia ushindi finyu dhidi ya Prisons. Naomba niwaeleze ukweli kuwa wanawaonea bure makocha na wachezaji wa Simba kwani hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kusubiri dakika 90 ziishe waondoke na pointi tatu kwa kutumia goli lile lile moja

Kama Prisons hawa wangepata sare au hata ushindi leo kisingekuwa kitu cha ajabu kwani nidhamu waliyoionyesha uwanjani ni ya kiwango cha juu mno hasa kwenye eneo la ulinzi. Mipango yote mizuri iliyofanywa na Hassan Dilunga kwenye kiungo ilifia kwa mabeki wa Wajelajela hao. .

Kama wataendelea kucheza katika nidhamu na kiwango kile ni wazi msimu huu wanaweza kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita. Kilichopelekea Simba ipate wakati mgumu ni kikosi cha Prisons kucheza kitimu zaidi kutokana na wachezaji wake kuzoeana (kikosi chao kina mabadiliko machache sana ukilinganisha na Simba). Msiilaumu Simba kupata ushindi mwembamba, ile Prisons ni timu na nusu.

Source :BOIPLUS MEDIA

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.