Azam Kumtangaza Mchezaji Mpya Leo.


Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza kuwa leo saa sita mchana itatangaza usajili wa mchezaji mwingine katika ofisi zao za Mzizima mbele ya Waandishi wa Habari.

Taarifa ambazo zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii mchana wa jana ni kwamba mlinzi wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amemalizana na Azam na ndiye atakaye tambulishwa hiyo leo.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema mchezaji atakaye tambulishwa ni Mtanzania lakini amegoma kumuweka wazi mpaka muda ukifika.

"Kesho saa sita mchana katika ofisi zetu za Mzizima tutatangaza usajili wa mchezaji wa pili tuliomsajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano mingine," alisema Jaffer.

Wiki iliyopita Azam ilimtambulisha mshambuliaji Donald Ngoma kutoka Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Jaffer amesema msimu ujao wamejipanga kufanya vizuri hivyo watafanya usajili mkubwa kutimiza azma hiyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.