Maka Edward hatatumia jezi namba 8 kwa msimu ujao anamuachia mchezaji mpya
Kiungo chipukizi wa klabu ya Yanga, Maka Edward amesema hatatumia jezi namba 8 kuanzia sasa kwa sababu anamuachia mchezaji mpya.
Hata hivyo, Maka hajamtaja jina mchezaji huyo mpya ajaye katika sehemu ndogo ya video iliyopostiwa kwenye akaunti rasmi ya Instagram, ya klabu ingawa miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa mbioni kusajiliwa ni kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa.
Kama ni Ngassa, ambaye kwa sasa anachezea Ndanda FC ya Mtwara atakuwa anajiunga na Yenga kwa mara ya tatu baada ya awali kuchezea kwa awamu mbili na kwa mafanikio.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.