Nsajigwa Amkingia Kifua Kamusoko


Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga SC Shadrack Nsajigwa amesema kuwa inabidi wawe na uvumilifu juu ya Kiungo wao Thaban Kamusoko kurejea Katika kiwango chake.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Zimbabwe anaesifika kwa pasi za kampa kampa tena Alicheza dakika 70 tu dhidi ya Kagera Sugar siku ya Ijumaa na kutolewa Katika Mchezo wake wa kwanza tokea takribani Miezi Mitano Kutoka katika Majeruhi.
"Ni vema tumemuona kurejea Katika timu hili ndio jambo jema,pili karejea Katika Kipindi kigumu na kizuri Katika ligi Kuu hatua ambayo tupo kuwania ubingwa ambao tunaushikiria sisi".

 
" Jambo jema ni kumpa muda na Sisi Viongozi pamoja na Mashabiki kuwa na uvumilivu wa kumsubiri arejee Katika kiwango chake kwani ni muda mrefu sana kakaa nje ya uwanja".Alisema kocha huyo Msaidizi wa Yanga Nsajigwa katika mahojiano na waandishi wa habari.


Thaban Kamusoko Ambae amerejea Kutoka Katika Majeruhi Siku ya Ijumaa Alianza Katika Kikosi cha kwanza kilichocheza dhidi ya Kagera Sugar Ligi Kuu Bara.

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.