Kessy Kuwakosa Township Rollers Mchezo Wa Marudiano..


Beki wa kulia wa Yanga Hassani Kessy ataukosa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers kutokana na kuwa na kadi mbili za njano

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema Kessy hataruhusiwa kucheza mechi hiyo kutokana na kuzuiwa na kanuni.

Alisema Kessy alipata kadi ya kwanza katika mchezo wa marudiano nchini Shelisheli dhidi ya St Luois kisha nyingine dhidi ta Township Rollers ya Botswana jumanne wiki hii.

"Tumeshaambiwa hatuwezi kumtumia Kessy katika mchezo wa marudiano, amefikisha kadi mbili za njano. Wachezaji wengine wako vizuri hakuna mwenye tatizo kama hilo, lakini tuna watu wa kuziba nafasi yake," alisema Saleh aliyedumu na Yanga kwa muda mrefu katika nafasi hiyo.

Tayari kocha, George Lwandamina ameanza kumuandaa beki mkongwe Juma Abdul kuziba nafasi ya Kessy.

Katika mechi yao ya kwanza iliyopigwa wikiendi iliyopita, Yanga ililala mabao 2-1 na kuwa na mlima wa kupanda wakati watakaporudiana wiki ijayo, ikihitaji kushinda ili kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.