Yanga kuungana na Simba kwa hili

Yanga kuungana na Simba kwa hili

Yanga imethibitisha kuwa itashiriki michuano ya SportsPesa Super Cup itakayofanyika Nairobi Kenya kuanzia Juni 3 hadi Juni 10, 2018.

Timu nyingine ambazo zitashiriki michuano hiyo ni pamoja na bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba na Singida United.


Bingwa wa SportPesa Super Cup atazawadiwa dola za Kimarekani kiasi cha elfu thelathini pamoja na kupata nafasi ya kwenda nchini Uengereza kucheza na klabu ya Everton ya nchini humo, safari ambayo itagharamiwa na SportPesa.

Wakati Tanzania visiwani inatoka timu ya JKU (itashiriki kama mwalikwa), huku Kenya ikishrikisha timu za Gor Mahia na AFC Leopard ambazo zilishiriki msimu uliopita michuano iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Gor Mahia ndio bingwa wa msimu uliopita baada ya kuitandika AFC Leopard katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Sports pesa ndio mdhamini wa vilabu hivyo vitano kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Simba, Yanga, Singida United, Gor Mahia na AFC Leopard.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.