Mbonde Ampa Matumaina Lechantre


Kurejea kwa beki Salim Mbonde kumerejea matumaini zaidi kwa Kocha Mfaransa wa Simba, Pierre Lechantre.

Lechantre anaamini sasa kikosi chake kimezidi kuimarika na kuongezeka kwa ushindani katika kusaka namba.

Simba itakuwa na kazi ya kuivaa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa keshokutwa Jumatatu.


Simba itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kucheza na Mtibwa mechi ya Ligi Kuu Bara ambapo katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Simba ina pigo la kuwakosa wachezaji watatu Juuko, Erasto Nyoni  na James  Kotei, hivyo kocha huyo anaamini Mbonde, atakuwa na nafasi ya kufanya vema.


Lechantre amesema suala la kuwakosa nyota wake hao watatu halimuumizi kichwa kwa sababu kuna wachezaji wengine wapo na watachukua nafasi zao.

“Ninaowakosa najua lakini nina imani na waliopo," alisema.

Mbonde ambaye amerejea anaweza kuwa na nafasi ya kushirikiana na Yusuph Mlipili katika safu ya ulinzi siku hiyo.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.