Mabadiliko ya ratiba VPL, Simba na Yanga kukutana Tarehe Hii
Bodi ya ligi kuu soka Tanzania Bara imefanya mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu ikiwa ni pamoja na kuzipa tarehe mechi ambazo hapo awali ziliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Katika mabadiliko hayo, mechi ya Njombe Mji na Simba ambayo awali iliahirishwa ili kuwapa nafasi Simba kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kufanyika April 3, 2018 katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe ukiwa ni mchezo nambari 171.
Kadhalika mechi inayowakutanisha Mbao FC na Lipuli FC itachezwa April 6 katika uwanja wa CCM Kirumba baada ya terehe ya awali kuonesha kuwa uwanja Utakuwa na matumizi mengine.
Mechi namba 183 inayowakutanisha wachimba Almasi Mwadui FC na Wanalizombe Majimaji FC itafanyika April 7, 2018 katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watarejea tena uwanjani April 9, 2018 kucheza na WanatamTam Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Mechi nyingine zilizorekebishwa ni ile Kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda FC ambayo itafanyika April 12 katika uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro, huku mechi ya Simba na Mbeya City nayo ikifanyika April 12, 2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Aidha Simba watacheza na Tanzania Prisons April 16, 2018 katika mchezo mwingine ambao umefanyiwa mabadiliko, ukifanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, na April 20, 2018 Simba watasafiri hadi Iringa kucheza na Lipuli katika uwanja wa Samora.
April 28, 2018 Majimaji watacheza na Ruvu Shooting mkoani Ruvuma, huku Mtibwa wakichuana na Azam katika uwanja wa Manungu, Stand United watacheza na Kagera Sugar.
Simba SC vs Yanga
Mechi ya watani wa Jadi ambayo awali ilipangwa kufanyika April 4, sasa itafanyika April 29 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Huku April 30, 2018 Mwadui FC watacheza na Mbao FC.
Mei mosi mwaka huu Yanga watasafiri hadi mkoani Mbeya kucheza na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine, Huku Mei 5, 2018 Yanga watarejea Dar kucheza na wabishi Mbao FC.
Mei 6, 2018 Kagera Sugar watacheza na Mbeya City katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Majimaji FC na Mtibwa Sugar, huku Simba wakicheza na Ndanda FC.
Mei 12, 2018 Mwadui FC watacheza na Yanga, Huku mechi ya Singida United na Simba ikifanyika Mei 11, 2018 katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Vilevile Mei 9, 2018 kutakuwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Yanga mechi ikifanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, Mei 16 Tanzania Prisons watacheza na Yanga.
Mei 19, 2018 Simba watawakaribisha Kagera Sugar, Mei 20 Azam watacheza na Tanzania Prisons, Yanga SC na Ruvu Shooting.
Kuhusu Matumizi ya uwanja wa Taifa, Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema mechi zote zinazowahusu Simba na Yanga zitafanyika kwenye uwanja wa Taifa isipokuwa mechi ya mwisho kati ya Yanga na Azam ambayo itafanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.