Tamko La Manara Baada Ya Wambura Kumuhusisha Kwenye Kesi Yake Dhidi Ya TFF


Mvutano mpya umeibuka baada ya aliyekuwa Makamu Rais wa TFF, Michael Wambura kumtumia Msemaji wa Simba, Haji Manara katika moja ya picha zinazosambaa kama kauli yake.

Kauli hiyo inaeleza makosa kadhaa ya Rais wa TFF, Wallace Karia kama kuruhusu mambo kuendeshwa kienyeji ikiwa ni pamoja na waliokuwa wanatumikia adhabu kuruhusiwa kufuata utaratibu uliowaondolea adhabu kinyume cha katiba ya TFF.

Wambura amemtaja Manara na Dk Damas Ndumbaro, jambo ambalo limemfanya Manara naye kujibu mapigo akimtaka Wambura amalizane na TFF na si yeye, huku akisisitiza “anaujua mziki wake”.

“Michael Wambura usinichokoze na usitafute huruma kupitia migongo ya watu,” anaandika Manara.

Anaendele: “Wala usimzushie Rais katika shauri langu na TFF, mimi sio maji yako nadhani unanijua vizuri. …Vita hii hainihusu ila unalazimisha kununua ugomvi, nikufahamishe tu kuwa shauri langu sikukuta rufaa, niliomba review sababu sikupewa nafasi ya kusikilizwa na huyo wakili wako (Emmanuel Muga), ndiye alishiriki kunihukumu bila kusikilizwa leo mnapata wapi moral authority ya kulalamika?”

“Watu mlioshiriki kutuonea wenzenu!! Nakuweka kiporo ukiendelea utachokoza jeshi la mtu mmoja litakaloeleza mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.”

Wambura amefungiwa kujihusisha na soka maisha ikiwa ni baada ya kupatikana na hatia ya kugushi baadhi ya nyaraka na kuchukua fedha zilizoelezwa ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo Wambura amekata rufaa kupinga mchakato mzima uliotumika kumfungia.

Lakini tayari Kamati ya Utendaji ya TFF, imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi ya Wambura.

SalehJembe Blog

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.