Buswita Kukabidhiwa Mikoba Ya Chirwa Huku Wawili Wakiondolewa Kikosini Yanga.


Kiungo mshambuliaji Pius Buswita huenda akaongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo wa leo dhidi ya Welayta Dicha.

Yanga ambayo ilirejea mapema jana ikitokea Morogoro ilikokuwa imeweka kambi ya siku tatu kujiandaa na mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wakati Amissi Tambwe akiondolewe kabisa kikosini, Donald Ngoma ana uwezekano mdogo wa kucheza mchezo huo (50/50).

Ikumbukwe Obrey Chirwa hatacheza mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano sambamba na Kelvin Yondani, Said Juma na Papi Tshishimbi.

Kwa hali hiyo kocha George Lwandamina atalazimika kumtumia Buswita kama mshambuliaji na haitakuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo kucheza nafasi hiyo msimu huu.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo licha ya kukosekana wachezaji wake muhimu.

Msimu huu Yanga imekuwa ikikumbana na changamoto za hapa na pale katika kikosi chake lakini jambo jema ni kwamba imekuwa ikifanya vizuri.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.