Lwandamina aenda na mzimu wa Yanga Zesco United

Lwandamina aenda na mzimu wa Yanga Zesco United

Baada ya kuondoka aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga George Lwandaminakama ameacha majanga katika klabu hiyo maana haijashinda hata mechi moja.

Sasa naye hapo jana imeanza vibaya na timu yake mpya Zesco United katika ligi ya Mabingwa barani Afrika.


Etoile Sahel timu kutoka Tunisia imeweza kuichabanga mabao 2-1 katika hatua ya makundi katika kundi D.

Katika mchezo wa kwanza Zesco United ilitoa sare 1-1 dhidi ya Swallows.

Hii imekuwa kama mwendelezo wa timu yake ya zamani Yanga kufanya vibaya katika michuano ya nje na ndani naye amepokea kijiti hicho akipokea kipigo.

Kwa matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao wa zamani wa Afrika, Etoile kuuungana na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye usukani wa kuongoza kundi hilo la D ikiwa timu zote zimejikusanyia alama nne.

Wakati klabu ya Zesco United ikiangukia nafasi ya tatu huku Primeiro Agosto ya Angola ikiburuza mkia.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.