Tetesi Za Usajili Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara Vodacom Premier league 22/05 /2018



Stand United imeripotiwa  kuanza mazungumzo na mshambuliaji wa Ndanda fc tiber John ili kuimarisha safu ya ushambuliaji pia na klabu ya yanga imemtolea macho mshambuliaji huyo wa Ndanda fc tiber John

 Singida United na klabu ya Simba Sc pia imeripotiwa kuwa wapo tayari kuanza mazungumzo na nyota anaye kuja kwa kasi Adam salamba taarifa za awali zinasema kuna uwezekano mkubwa sana wa kutua katika klabu ya Singida United

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Simba sc Laudit Mavugo huenda akatemwa katika kikosi cha Simba sc hii inatokana na kushuka kiwango taarifa zinasema Mavugo huenda akatimkia katika klabu ya yanga sc

Hans van der Pluijm taarifa kutoka ndani ya Singida United zinasema kuwa tiyari wamefikia muafaka na tiyari ruksa kuondoka katika klabu ya Singida United na taarifa za awali van der Pluijm yupo mbioni kujiunga na matajiri wa jiji la Dar es Salaam waoka mikate Azam FC

Klabu ya yanga huenda ikaachana na baadhi ya nyota wao wa kimataifa kwa sababu mbalimbali na tiyari klabu ya yanga imeanza mazungumzo na kiungo wa Don bosco ya nchini Congo cadrick kabale pamoja na alain mulumbe anayekipinga klabu ya motema pembe

Mohamed Ibrahim Mo naye yupo mbioni kutimka katika klabu yake ya Simba Sc na bado haijafahamika rasmi atatimkia klabu ipi lakini taarifa za awali zinasema huenda akahamia katika klabu ya yanga sc

@bwajideo

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.