NYOTA SINGIDA UNITED WALIOSHINDWA KUFANYA VYEMA MSIMU HUU.


BENCHI la ufundi la Singida United limesema wachezaji wa kimataifa hasa katika safu ya ushambuliaji msimu huu wameshindwa kuitendea haki klabu hiyo msimu huu jambo ambalo limeifanya kuwa nje ya malengo iliyojiwekea.


 Kilio kikubwa cha Singida United kimekuwa kwa mastraika wake, Danny Usengimana, Lubinda Mundia na Sanita Kambale ambao kwa pamoja wameshindwa hata kuifungia timu hiyo mabao 15 licha ya kusajiliwa kwa gharama kubwa na kulipwa fedha nyingi.


Kocha Msaidizi wa Singida United, Jumanne Challe alisema wachezaji hao wameonyesha kiwango cha kawaida tofauti na walivyokuwa wanatarajia kabla ya kuwasajili.Alisema wachezaji hao wamekuwa wakipata nafasi nyingi za kufunga lakini wanashindwa kuzifanyia kazi hivyo kuifanya timu yao ipate matokeo mabovu.

“Kiujumla hawakuwa na msaada mkubwa kwa timu kutokana na kushindwa kufunga mabao mengi ambayo yangeweza kuibeba timu kwa namna moja au nyingine,” alisema.


Nyota wengine wa kigeni waliosajiliwa na timu hiyo ni Elisha Muroiwa Malik Antri, Shafiq Batambuze ambao amewapa sifa kuwa ni wachezaji wazuri lakini kwa nyakati tofauti wameshindwa kuisaidia timu kufikia malengo waliyokusudia kabla ya msimu kuanza.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.