Msuva Atua Kambini Yanga Nchini Algeria
Winga wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga Difaa El Jadida ya Morocco, Saimon Msuva mapema jana alifika kambi ya Yanga jijini Algiers kuwapa moyo vijana wanaotarajia kushuka dimbani kuwakabili USM Algiers.
Difaa El Jadida ilikuwa nchini Algeria kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mouloudia Club D'Alger.
Mchezo huo ulicheza juzi Ijumaa usiku na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 Msuva akicheza kwa dakika 87.
Msuva aliyejiunga na timu hiyo ya Morocco akitokea Yanga msimu uliopita, amekuwa mchezaji wa kutegemewa wa kikosi cha kwanza.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.