Kocha Yanga Kuishuhudia Timu Yake Akiwa Jukwaani.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ataishuhudia timu hiyo jukwaani itakapokuwa ikiikabili USM Alger kwenye mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la Shirikisho Barani Afrika kutokana na kutokamilika kwa vibali vyake.
Zahera amesafiri sambamba na makocha wasaidizi Shedrack Nsajigwa na Noel Mwandila ambao ndio watakuwa na majukumu ya kukiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo huo.
Kocha huyo alitua Yanga wiki mbili zilizopita kuchukua nafasi ya George Lwandamina ambaye ametimkia ZESCO FC.
Mpaka wakati Yanga inaondoka kwenda Algeria vibali vya kocha huyo vilikuwa havijakamilika

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.