Nyota 10 Yanga Hatihati Kuondoka..
Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzania, Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kuamua hatma ya wachezaji hao.
Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika ni pamoja na Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Juma Abdul, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa.
Wengine ni Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.