Niyonzima Afunga Bao La Kwanza Tangu Ajiunge Na Simba Na Bao Hilo Laishusha Daraja Majimaji FC
Kiungo Haruna Niyonzima amefunga bao la kwanza tangu asajiliwe na Simba katika mchezo wa kufungia msimu dhidi ya Majimaji uliomalizika kwa sare ya bao moja.
Niyonzima alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 45 baada ya Rashid Juma kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Raia huyo wa Rwanda alikuwa hajaifunga bao lolote tangu aliposajiliwa kutoka Yanga mwanzoni mwa msimu huku akiandamwa na majeruhi.
Mshambuliaji Marcel Kaheza aliifungia Majimaji bao la mapema dakika ya sita baada ya kutumia uzembe wa walinzi wa Simba.
Matokeo hayo yameifanya Majimaji kushuka daraja baada ya kumaliza nafasi ya pili kutoka kutoka chini wakiwa na pointi zao 25 wakiwafuata Njombe Mji ambao walishuka mapema.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.