Lipuli Waigomea Yanga Kwa Salamba

sokakiganjani blog
Hatimaye klabu ya Yanga imekosa rasmi huduma ya mshambuliaji Adam Salamba wa Lipuli FC kufuatia kanuni za soka kukataa.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Katibu mkuu wa klabu hiyo, Amos Lweramila imesema katiba ya FIFA,  CAF na TFF hairuhusu mchezaji kucheza timu tatu ndani ya msimu mmoja.

Msimu Salamba amechezea timu za Stand United na Lipuli hivyo kanuni hairuhusu kucheza tena Yanga.

"Kweli tumepokea barua kutoka timu ya Yanga ikitaka kumuazima mshambuliaji wetu Adam Salamba katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika lakini kanuni za FIFA, CAF na TFF zinakataa.

"Kanuni zinataka mchezaji kucheza timu mbili ndani ya msimu mmoja na Salamba amecheza Stand na Lupuli kwahiyo hawezi tena kucheza Yanga," alisema Katibu huyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.