Taarifa Mpya Kutoka Yanga Usiku Huu...


Taarifa Kutoka Yanga SC ni Kuwa kikosi cha Yanga kitawafuata timu ya Mwadui Fc kesho Alfajiri na jumla ya wachezaji 20 na viongozi 8. Yanga Watacheza na Mwadui siku ya Jumamosi may 19 katika dimba la CCM kambarage mkoani Shinyanga kuanzia majira ya saa10:00 jioni.

-Jana Klabu ya Yanga Sc walicheza mchezo wa kombe la shirikisho na Rayon Sports ya Rwanda na kutoa suluhu ya bila kufungana. Wachezaji wawili waliocheza jana watakosekana kwenye msafara wa  kesho kutoka na sababu mbalimbali, Ramadhani Kabwili leo alitarajiwa kuondoka kuwafuata timu ya Ngorongoro Heroes Mali kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Mali u20 kikosi cha Ngorongoro Heroes waliondoka jana.

-Pia Kelvin Yondani amefungiwa kucheza ligi kuu Tanzania Bara kutokana na kumtemea mate mchezaji wa Simba, Asante Kwasi na suala lake halijatolewa na maamuzi na kamati ya nidhamu baada ya Kelvini Yondani kushidwa kutokea kwenye kamati.

-Ukiacha wachezaji walio majeruhi na wengine ambao hawakuwepo kambini wachezaji  wengine wote wataenda Mkoani Shinyanga na kocha mkuu wa klabu Hiyo Mwinyi Zahera ataongozana na kikosi hicho baada ya kucheza mchezo huo watarudi jijini Dar kucheza mchezo na Mbao Fc may 22 katika uwanja wa Taifa jijini Dar. Orodha ya wachezaji wote 20 itajulikana kesho asubuhi.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.