Kumbe Mkemi Hajajiuzulu Yanga
Pamoja na kuenea kwa taarifa kwa Mjumbe wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amejiuzulu, imeelezwa bado anaendelea kuitumikia klabu hiyo.
Mmoja wa viongozi wa Yanga, aaiongea na SALEHJEMBE amesema kwamba pamoja na ukimya lakini Mkemi bado yuko Yanga.
“Bado tupo na Mkemi na tunaendelea vizuri kabisa,” alieleza.
“Huenda watu wamesikia wakaamini, maana niliposikia nikazungumza naye na kasema hana huo mpango.”
Mkemi ni kati ya viongozi vijana wanaoiongoza Yanga na wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kuandamwa na ukata.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakishinikiza ajiuzulu jambo ambalo yeye bado hajapatikana kulizungumzia
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.