Hawa ndiyo mabeki 5 bora wa pembeni ligi kuu Tanzania

Ligi kuu ya Tanzania bara inaisha jumatatu ambapo michezo yote itapigwa wakati mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu na mkali ule wa Yanga na Azam utakaopigwa katika dimba la taifa Dar es Salaam.
Baada ya kuona kikosi bora cha mwaka sasa hawa ni mabeki bora wa pembeni kwa msimu wa ligi kuu Tanzania bara kutoka katika vilabu vyote bali hapa wamechaguliwa watano.
Asante Kwasi
Beki huyu anasifa ya kucheza kati lakini tangu atue Simba amekuwa akitumika kama beki wa pembeni hivyo, wakati anacheza Lipuli amepachika mabao 5, baada ya kutua Simba ameongeza magoli mawili.
Uwezo wake wa kupanda kushambulia pamoja na kurejea kuzuia ndio sababu ya kuingia katika orodha hii ya mabeki bora. Pia amefunga magoli 7 ambayo hata washambuliaji wengine hawajafika.
Gadiel Michael
Wakati usajili wake kutoka Azam kulikuwa na utata baada ya kufosi kuondoka Azam hii baada ya kusikia kuhitajika Yanga.
Ujio wake umeweza kumuweka benchi Haji Mwinyi ambaye alitengeneza ufalme wake katika klabu hiyo.
Gadiel Michael alifunga goli la kihistoria tena akiitungua timu yake ya zamani Azam na miongoni mwa goli litakalo gombania goli bora, kwa nafasi yake anastahili kuwa katika nafasi hii katika kikosi cha mwaka.
Shafik Batambuze
Singida United wameweza kuangalia mchezaji gani ataweza kuwasaidia, bila shaka uwezo wake umedhihirika katika ligi kuu Tanzania bara, alifanya vizuri sana katika michuano ya  Mapinduzi, uwezo wake wa kupiga pasi makini pamoja na kufugna pia ameweza kuhesabika kama beki bara Tanzania 2017-2018.
Hassan Kessi
Anapokuwa uwanjani anajitolea kwa hali na mali kuweza kuisaidia timu yake uwezo huu aliuonesha tangu yupo Simba baadaye alipofika Yanga amemuweka benchi Juma Abdul nakuwa msaada katika timu hiyo.
Anauwezo wa kupanda na kushuka anachangamsha mashambulizi, tatizo lake kubwa kulalamikia waamuzi  akiacha hilo miongoni mwa watu watakaofanya vizuri sana.
Shomary Kapombe
Shomary moja ya wacheaji waliokuwa na uwezo wa hali ya juu, ukweli ni kwamba majeruhi yanamtatiza sana, licha ya kuikuta ligi katikati bado anauwezo wa kuwazidi mabeki wengine. Ameweza kutoa pasi za mwisho na madhara yake yanaonekana. Erasto Nyoni hatujamuweka kwa kuwa anacheza namba nyingi na anastahili kuwa mchezaji bora msimu huu.
Unaweza kuchangia kupitia kurasa zetu za facebook,Instagram na Twitter ukiandika azaniapost, sema kikosi chako.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.