Mo Salah Anyakuwa Tuzo Ya Mchezaji Bora.
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwamwezi Machi baada ya kuendelea kufanya kazi nzuri Liverpool.
Hii inakuwa nara ya tatu kwa msimu huu pekee nyota huyo wa Misri huyo kutwaa tuzo hiyo, baada ya kuchukua pia miezi ya Novemba mwaka jana na Februari, mwaka huu.
Tangu amerejea England msimu huu akijiounga na kikosi cha Jurgen Klopp cha Liverpool, mchezajhi huyo mwenye umri wa miaka 25 anaonekana mchezaji tofauti kabisa na yule aliyekuwa Chelsea ya hapa pia, kati ya mwaka 2013 na 2015
Salah pia amevunja rekodi ya Didier Drogba ya mchezaji kutoka Afrika kufunga mabao mengi kwa msimu baada ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salaam, Uwanja wa Selhurst Park dhidi Crystal Palace.
Naye kocha wa Burnley, Sean Dyche ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Machi, wakati Jamie Vardy wa Leicester City ameshinda tuzo ya Bao Bora la Mwezi Machi.
Dyche ameiwezesha Burnley kushinda mechi zake zote za mwezi akianza na Everton, West Ham na West Brom, wakati Jamie Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya vao lake zuri alilofunga dhidi ya West Bromkwch Albion kwenye ushindj wa 4-1 Machi 10
Washindi wengine waliotangulia hapo awali.
August - Sadio Mane
September - Harry Kane
October - Leroy Sane
November - Mohamed Salah
December - Harry Kane
January - Sergio Aguero
February - Mohamed Salah
March - Mohamed Salah
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.