HUU NDIO MPUNGA ATAKAO LIPWA KOCHA HANS AKIWA NA AZAM FC..
-Klabu ya Azam imemalizana na kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm na atakuwa kocha mkuu wa klabu hiyo msimu ujao. Azam tayari wameachana na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Aristica Cioaba.
-Babu Hans atasaini mkataba wa miaka miwili Azam ambao atakuwa analipwa tsh milioni 24 kwa mwezi na atakuwa kocha wa pili kwa makocha wa ligi kuu Tanzania Bara (vpl) wanaolipwa mkwaja mrefu nyuma ya Pierre Lechantre.
-Hans atakuwa analipwa tsh 800,000 kwa siku, huku kwa saa ikiwa ni tsh 33,333.33 na kwa dakika atakuwa anakunja tshs 555.55 pia atakuwa anapewa bonasi kwa kila mechi ikiwa timu ikishinda au kutoa sare pia kuna bonas iwapo timu itakuwa bingwa wa vpl.
-Klabu ya kuondoka kocha wa Yanga, George Lwandamina ndio alikuwa napokea mpunga mrefu kuliko wote alikuwa analipwa milioni 36 kwa mwezi kwa sasa kocha wa Simba, Pierre Lechantre ndio anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa analipwa milioni 30 kwa mwezi huku kocha wa Yanga Mwinyi Zahera akiwa kocha wa tatu kwa kulipwa mshahara mkubwa akiwa analipwa milioni 12 kwa mwezi.
@yossima Sitta Jr.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.