Amka Na Habari Hii Mpya Kutoka Simba sc.

sokakiganjani blog

Kikosi cha mabingwa wa ligi kuu bara timu ya Simba kinatarajia kuondoka leo kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji wiki ijayo.

Mchezo ni muhimu zaidi kwa Majimaji kwani wapo nafasi ya pili kutoka mwisho na ushindi ukiwa ndio njia pekee ya kuwabakiksha msimu ujao huku wakiiombea mabaya Ndanda katika mchezo wao dhidi ya Stand United.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Manara amesema kikosi kipo kamili na wanatarajia kufanya vizuri katika mchezo huo.

Manara alisema wanatarajia mchezo mgumu kutoka kwa Majimaji kwakua wapo katika hali mbaya lakini wamejipanga kuondoka na alama zote tatu.

"Kikosi kinaondoka kesho kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho msimu huu dhidi ya Majimaji kikiwa katika hali nzuri," alisema Manara jana.

Ligi kuu bara itamalizika Jumatatu Mei 28 kwa timu zote 16 kushuka dimbani katika viwanja tofauti huku mechi zote zikianza pamoja.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.