KWAHERI NJOMBE MJI TUTAONANA FDLMSIMU UJAO


KLABU ya soka ya Njombe Mji ya mjini Njombe, imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi kuu hadi Lidi daraja la kwanza kwa msimu ujao wa 2018-19 baada ya kushiriki VPL kwa msimu mmoja pekee.

Njombe wameshuka kufuatia kichapo walichokitoa Ndanda kwa Mwadui FC cha mabao 3-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na kufikisha pointi 26 ambazo Njombe hawawezi kuzifikia hata kama watashinda mchezo wao wa mwisho May 28

Vibonde hao wa Njombe wamejikusanyia pointi 22 baada ya kucheza michezo 29 ikiwa ni pointi mbili nyuma ya Majimaji ambao pia wanahali tete na wanatarajia kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya mabingwa wapya wa VPL Simba SC siku ya Jumatatu ya My 28 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji huko mjini Songea.

Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) zinataraji kushuka timu mbili ili kupisha ingizo la timu sita msimu ujao wa 2018-19 na kutimiza idadi ya timu 20 katika ligi ya msimu huo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.