THOMAS ULIMWENGU ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI NA AL HILAL YA SUDAN.
Klabu ya Al Hilal ya Sudan imeingia mkataba na mchezaji, Mtanzania, Thomas Ulimwengu, kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu.
Al Hilal imemsajili Ulimwengu kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili tayari kuanza kukipiga ndani ya Waarabu hao.
Timu hiyo imeshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi nchini humo ikiwa imejikusanyia pointi 33 katika michezo 33 iliyocheza.
Ulimwengu amejiunga na Al Hilal baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza soka tangu aachane na timu ya AFC Eskilstuna ya Sweden aliyokuwa akiitumikia.
Winga huyo pia aliwahi kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Congo sambamba na Mshambuliaji Mtanzania mwenzake anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji hivi sasa, Mbwana Samatta.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.